MAHITAJI
- 360 gram peanut butter.
- 1 kg high quality chocolate chips, milk chocolate nzuri kwa familia.
- 360 gram sukari ya unga [ icing sugar]
- 6 kijiko kikubwa cha chakula siagi iliyoyeyushwa
- Cooking Spray
- Mini Cupcake Papers.
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
→Haya ni maandalizi ya vitu vyote unavyohitaji kwa kutengeneza kitafunwa hiki.
→Yeyusha siagi kwenye microwave.
→Kisha chukua peanut butter weka kwenye bakuli safi na kisha changanya na icing sugar pamoja na vijiko 4 vya siagi liyoyeyushwa.
→Ukiona bado ni kavu sana ongeza vijiko viwili vilivyobakia.
→Endelea kukoroaga upate mchanganyiko laini.
→Yeyusha chocolate kwenye microwave hakikisha unaikoroga koroga mara kwa mara mpaka itakapo yeyuka nikiwa na maana weka dakika 1 toa koroga kisha rudisha kwenye microwave kwa dakika 1 toa koroga mpaka iyeyuke na kua laini kabisa.
→Panga hizo cupcake papers kwenye tray ya kuokea baking sheet paka mafuta ya siagi hizo cupcake zote mimi huwa natumia spray special.
→Chukua chocolate iliyoyeyuka kisha mimina kijiko kimoja tu kwenye cupcake papers, hakikisha imeenea vizuri kwa chini.
→Tumia kidole chako kuisambaza vizuri na uhakikishe imeshika vizuri kabisa.
→Fanya hivyo kwa cupcake zote na hakikisha mchanganyiko wa chocolate umebaki pembeni kwajili ya matumizi mengine.
→Baada ya kumaliza zoezi hili, chukua tray weka kwenye friji ipoe kwa dakika 5 hadi 10.
→Baada ya dakika 5 hadi kumi utapata muonekano huu na chocolate itakua imeganda.
→Chukua piping bag au mfuko wa nailoni na kisha tumia glasi kwa kukusaidia kumiminia mchanganyiko wao wa peanut butter kwa urahisi tumbukiza mfuko wako ndani ya glasi na kisha anza kumimina mchanganyiko wa peanut butter.
→Kisha anza ku Pipe au unaweza kutumia kijiko kuweka mchanganyiko wa peanut butter kwenye chocolate cups zilizotoka katika friji.
→Tumia piping bag ni nafuu na haraka zaidi!
→Huu ndio muonekano baada ya kuweka peanut butter katika chocolate cupcakes
→Tumbukiza kijiko chako kwenye maji na kisha kandamiza moja baada ya nyingine kutengeneza umbo zuri.
→Chukua chocolate iliyobakia iliyokwisha yeyushwa na mimina juu ya peanut butter na urudishie tray kwenye friji kwa dakika 30 iweze kukamilika kabisa.
→Recipe nzima inaweza kutoa vipande 55 mini peanut butter cups.
→Baada a dakika 30 itakua imeset safi kabisa na tayari kuliwa.
→Ukitoa kwenye cup cakes utapata muonekano huu safi sana.
WASILIANA NA WATAALAMU HUSIKA.
Email: issakesu@gmail.com