- 250 gram unga wa ngano.
- 120 gram unga wa mchele.
- 1 kijiko kidogo cha chai hiliki ya unga au unaweza saga mbegu ikawa chenga. chenga
- 120 gram sukari.
- 120 gram maji ya vugu vugu.
- Nusu kijiko kidogo cha chai amira ya chenga.
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
→Chukua maji ya vugu vugu changanya na amira ya chenga, sukari pamoja na hiliki.
→Chukua unga wa ngano na unga wa mchele changanya pamoja.
→Chukua mchanganyiko wa maji mimina kwenye mchanganyiko wa unga wa ngano na mchele na kisha tumia mwiko kukoroga pole pole mapaka ichanganyike vizuri.
→Kama mchanganyiko wako ni mwepesi sana basi unaweza tumia mayai au ukaongeza maji au maziwa kiasi hakikisha mchanganyiko huu usiwe mwepesi kabisa na usiwe mzito sana ubora uwe kama unavyoona kwenye picha hapo juu.
→Chukua kikaango cha vitumbua kisha weka mafuta ya kupikia kijiko kimoja kidogo cha chai.
→Mafuta yakisha pata moto mimina mchanganyiko wako wa unga wa mchele kwenye kikaango.
→Ukishaona rangi ya kahawa kwa chini basi geuza upande wawili na weka mafuta tena.
→Mpatie mlaji chakual kikiwa cha moto atafurahi sana.
→Huu ni muonekano safi kabisa wa kitumbua hiki chenye mchanganyiko wa unga wa aina mbili safi sana kwa kitafunwa cha nyumbani na restaurant.
WASILIANA NA WATAALAMU HUSIKA
Email: issakesu@gmail.com