MAHITAJI
- Sukari vikombe 2.
- Maji vikombe 2.
- Nusu kikombe unga wa ubuyu.
- Vikombe 4 ubuyu wenyewe.
- 1/4 tps pili pili ya unga.
- 1/4 tsp chumvi.
- 1/4 tsp iliki ya unga.
- Rangi nyekundu au yeyote ile utakavyopenda.
JINSI YA KUANDAA
→Katika sufuria,weka maji na sukari na chumvi na pili pili ya unga na Rangi na iliki.
→Moto uwe juu kiasi na changanya vyote hivyo vipike vizuri.
→Wakati vitu vinaanza kujipika utakuta rojo linatoa mapovu.
→Endelea tu kukoroga acha rojo lipikike vizuri.
→Baada ya hapo mapovu yakianza kutulia inamaanisha kua rojo limeanza kua zito.
→Sasa hapo chota kidogo katika mwiko na test kwa vidole kama rojo linanata ua halinati.
→Rojo linatakiwa linate ndio linakua limeiva.
→Lisinate sana kiasi tu.
→Kisha mimina ubuyu wa kokwa na changanya vizuri kabisa katika rojo.
→Endelea kupika vizuri kama dakika 2 hivi.
→Kisha mimina unga wa ubuyu na changanya vizuri tena.
→Endelea kupika mpaka unaona sukari inaanza kuganda na kung'aa na kushika vizuri katika ubuyu.
→Hapo sasa zima jiko na mimina ubuyu katika sinia kubwa na acha ubuyu upoe.
→Ukishapoa ubuyu tayari kuliwa.